Uko hapa: NyumbaniHabari2021 10 06Article 561625

Uhalifu & Adhabu of Wednesday, 6 October 2021

Chanzo: ippmedia.com

27 walioiba saruji kwenye ajali wakamatwa

27 walioiba saruji kwenye ajali wakamatwa 27 walioiba saruji kwenye ajali wakamatwa

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia watu 27 kwa tuhuma za kuiba saruji baada ya ajali ya malori mawili iliyotokea Mbagala Mission wiki hii.

Oktoba 4, mwaka huu katika eneo la Mbagala Mission ilitokea ajali ya malori mawili lenye namba T 164 DKC na T 342 DJZ lililokuwa limebeba saruji, ambapo lilitumbukia kwenye mtaro baada ya kupasuka tairi.

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Muliro Jumanne Muliro, alisema jana kuwa baada ya ajali hiyo zaidi ya watu 50 walijitokeza na kuiba mifuko ya saruji iliyokuwa imebebwa na gari lililopata ajali.

“Jana (juzi) majira ya saa 06:40 usiku eneo la Mbagala Mission, lori lingine lenye namba za usajili T 705 AUE lililokuwa na tela lenye namba za usajili T 911 ATR likiendeshwa na Muhidini Hussein (39), mkazi wa Morogoro, likitokea Mbagala kuelekea mjini likiwa limebeba zaidi ya mifuko 700 ya saruji nalo lilipata ajali,” alisema Muliro.

Aliongeza kuwa baada ya ajali hiyo Polisi walifika mapema katika eneo la tukio na kuwakuta watu 27 wakiwa wanaiba saruji kwa kuipakia kwenye pikipiki na bajaji. Na wote walikamatwa na jumla ya mifuko 368 iliokolewa ikiwamo 10 iliyokutwa kwenye nyumba za watu.

Muliro alisema watuhumiwa watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo, na kutahadharisha kwamba Jeshi la Polisi halitasita kushughulika kikamilifu kwa mujibu wa sheria na watu wote wenye tabia ya kukimbilia kwenye matukio ya ajali na kufanya wizi badala ya kuokoa watu na mali.