Uko hapa: NyumbaniInfos2020 09 25Article 510379

Crime & Punishment of Friday, 25 September 2020

Chanzo: Zanzibar 24

AKATAA KUMPELEKA MZAZI WAKE SHULENI, AMSHAMBULIA MWALIMU WAKE KWA PANGA

AKATAA KUMPELEKA MZAZI WAKE SHULENI, AMSHAMBULIA MWALIMU WAKE KWA PANGA

Mwanafunzi wa Kidato cha tatu Mwita Machamo, (17) wa shule ya sekondari ya Kiagata, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mara kwa kumkata na panga mwalimu wake Majogoro John, baada ya mwanafunzi huyo kushindwa kumpeleka mzazi wake shuleni kama alivyoagizwa na Mwalimu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Daniel Shillah amesema kuwa tukio hilo lilitokea shuleni hapo majira ya asubuhi wakati mwalimu anakagua wanafunzi watoro, na ndipo mwanafunzi huyo alimgeukia mwalimu wake na kumkata mapanga.

“Baadhi ya wanafunzi waliwaleta wazazi wao, lakini huyu mwanafunzi kwa utovu wa nidhamu uliopindukia alikuja na upanga akiwa ameuficha kwenye nguo zake na mwalimu alipohoji kwanini hujaja na mzazi, mwanafunzi akachomoa upanga na kumshambulia mwalimu na akawatisha tisha wanafunzi wengine akapata nafasi ya kukimbia lakini wakamkata na tumemshikilia na atafikishwa mahakamani” Kamanda Shillah

Join our Newsletter