Uko hapa: NyumbaniHabari2021 10 13Article 563092

Habari Kuu of Wednesday, 13 October 2021

Chanzo: tanzaniaWeb

ATCL yaanzisha safari za Bujumbura, Lubumbashi, Nairobi

ATCL yaanzisha safari za Bujumbura, Lubumbashi, Nairobi ATCL yaanzisha safari za Bujumbura, Lubumbashi, Nairobi

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limeongeza safari zake za ndani na nje ya Tanzania ikiwa ni kipindi kifupi baada ya ujio wa ndege mbili aina ya Airbus.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mahusiano ATCLJosephat Kagirwa amesema safari hizo mpya zinazotarajiwa kuanza Novemba, 2021.

Safari zilizoongezwa ni pamoja na Dodoma-Mwanza, Dar-Mtwara, Dar-Bujumbura, Dar-Lubumbashi pamoja na Dar -Nairobi.

Amesema safari za Dar-Mwanza zitaanza Novemba 5 na Dar kwenda Mtwara Novemba 8 na Novemba 18 ni Dar Lubumbashi-Bujumbura na safari za Nairobi zitaanza Novemba 26.

“Kutokana na ujio wa ndege mpya Airbus, ATCL tutafungua safari kwenda Andora Zambia, Bujumbura, Lubumbashi , safari hizi zinaanza November, pia ndani ya nchi route mpya itakuwa DSM kwenda Dodoma mpaka Mwanza, pia tunafungua safari za Mtwara baada ya Uwanja kuamaliza matengenezo” Josephat Kagirwa