Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 14Article 585808

Muziki of Friday, 14 January 2022

Chanzo: eatv.tv

AY avunja ukimya kuhusu mziki wa Amapiano

Ambwene Yesaya, Ay Ambwene Yesaya, Ay

Masta AY Tanzania 'Mzee wa Commercial' ameuliza kuhusu biashara ya muziki wa Amapiano kwa wasanii wa Tanzania nchini South Africa kama wao wanavyokuja kwa wingi kupiga pesa Tanzania.

Kupitia page yake ya Twitter AY ameandika kwamba "Wakuu, wasanii na Ma Dj's waliokuwa busy na kufanya Amapiano hapa Tanzania, mpaka leo nani kashaenda South Africa kuokota hela zao tujifunze biashara"

"Maana naona wasanii na dj's wa South Africa wanavyokuja kuokota hela Bongo,nini shida".