Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 13Article 551401

Uhalifu & Adhabu of Friday, 13 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Afariki kwenye mapigano ya polisi na wafugaji

Silaha za Jadi Silaha za Jadi

Mfugaji aliyetambulika kwa majina ya Julius Nyau, Mkazi wa Kijiji cha Mchomoro Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma, amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali kifuani na shingoni kwenye vurugu baina ya polisi na wafugaji wilayani humo.

Jeshi la Polisi mkoani humo limethibitisha kutokea kifo hicho na kueleza kuwa, walikuja kuwakamata watuhumiwa waliokuwa wanashambulia wakulima kwenye eneo la Pori la Nakayombo kijijini hapo.

Ndipo walipoaanza kuwashambulia Polisi kwa silaha za jadi , kitendo ambacho kilipelekea kuibuka kwa vurugu ambayo ilipelekea kifo cha mfugaji huyo.