Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 21Article 558766

Habari za Mikoani of Tuesday, 21 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Agizo la RC Makalla kwa hospitali zinazouia maiti kisa madeni

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesisitiza agizo lililotolewa na Wizara ya Afya linalokataza Hospitali kuzuia maiti kuchukuliwa na ndugu kwa kigezo cha deni.

Mkuu wa Mkoa huyo amesema hayo baada ya kupokea malalamiko toka kwa Wananchi kuwa bado kuna hospitali hazitekelezi agizo hilo la Wizara na Kuendelea kuzuia maiti mpaka zilipiwe fedha za matibabu zilizokwisha tumika.

Hata hivyo kitendo hicho kinapelekea vyumba vya kuhifadhia maiti kukosa nafasi kutokana na hospital nyingi kukatalia maiti.

Aidha, Makalla amewaelekeza Waganga Wakuu wa Wilaya kuhakikisha tatizo hilo halijirudii.