Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 29Article 540541

Uhalifu & Adhabu of Saturday, 29 May 2021

Chanzo: millardayo.com

Aiba mtoto kisa ndoa (+video)

Aiba mtoto kisa ndoa (+video) play videoAiba mtoto kisa ndoa (+video)

Jeshi la Polisi Mkoani Kagera limemkamata na linaendelea kumhoji Fatuma Joswamu ( 23) kwa tuhuma za kumuiba Hospitalini Mtoto mchanga mwenye umri wa siku 12 tu.

“May 24,2021 saa kumi usiku alifika Hospitalini akijaribu kuwaongopea Wauguzi kuwa ni mjamzito alifunga vitambaa tumboni wakampa kitanda, asubuhi yake saa 12:45 asubuhi jirani yake akaenda nje akaacha katoto kake kachanga Mtuhumiwa akakachukua na kuondoka nacho”———RPC Kagera

“Mama aliporudi na kumkosa Mtoto wake akatoa taarifa kwa Manesi wakajulishwa Walinzi na wakazingira Hospital na kumnasa Fatuma, tulipomuhoji anasema ameolewa na Mumewe muda mrefu lakini hawajapata Mtoto na Mumewe anadai Mtoto hivyo ili kulinda ndoa yake yenye mgogoro akajifanya ana mimba, akapanga tarehe za kujifungua ndio kama hivi aibe Mtoto, tunamuhoji upelelezi ukikamilika atafikishwa Mahakamani”———Revocatus Malimi, RPC Kagera.

Join our Newsletter