Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 03Article 540772

xxxxxxxxxxx of Thursday, 3 June 2021

Chanzo: millardayo.com

Ajali ya bus Shinyanga wawili ICU "Serikali itasimamia mazishi"

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itagharamia mazishi ya Watu waliofariki kufuatia ajali ya Basi la Kampuni ya Classic iliyotokea Shinyanga alfajiri ya leo wakati Basi hilo likitokea Uganda kuja Dar es Salam.

“Rais anawapa Ndugu wa Marehemu pole sana kwa msiba huu wa kuondokewa na Wapendwa wenu na Serikali itagharamia shughuli za mazishi” Hemed

Waliofariki kwenye ajali hiyo ni watatu wote kutokea Zanzibar (Rehema Haji Juma, Wahda Yussuf na Nassor Juma Khamis), waliotoka wakiwa wazima ni 14 , Majeruhi 10 wanaendelea na matibabu na wawili wapo ICU Bugando Hospital.

Join our Newsletter