Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 23Article 553072

Habari Kuu of Monday, 23 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Ajali yaua wafanyakazi watano wa TRA

Ajali ya wafanyakazi wa TRA Ajali ya wafanyakazi wa TRA

Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wamefariki dunia kwa ajali ya gari aina ya Landcluser lililogonga kwa nyuma Lori aina Fuso.Ajali hiyo imetokea leo Agosti 23, 2021, saa 11 alfajiri katika barabara ya Mbeya Tunduma eneo la Hanseketwa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.

Tayari Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kutaja idadi hiyo ya vifo, taarifa zaidi kutolewa na TRA.