Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 18Article 572452

Habari za Mikoani of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: mwananchidigital

Ajali za barabarani zapungua Tabora

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao

Ajali za barabarani mkoani Tabora zimepungua kwa asilimia 47 katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Juni hadi Oktoba mwaka huu, ikilinganishwa na miezi hiyo mwaka Jana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao,amesema leo kuwa, katika miezi hiyo mwaka jana kulikuwa na ajali 21 wakati kipindi hicho mwaka huu kuna ajali 11.

"Tumefanikiwa kupunguza ajali kwa kiwango kikubwa sawa na asilimia arobaini na Saba na tunataka tupunguze zaidi"Amesema

Kamanda Abwao ametoa sababu za kupungua ajali kuwa ni elimu inayotolewa kwa watumiaji wa barabara hasa watumiaji wa vyombo vya moto kama madereva bodaboda,magari na wapanda baiskeli pamoja na watembea kwa miguu ambapo elimu hiyo,imejikita kiwafundisha matumizi sahihi ya barabara.

Sababu nyingine ni wamiliki wa vyombo vya moto kuwa walihimizwa kuvifanyia matengenezo ya mara kwa mara ili kuviwezesha vyombo vyao kuwa imara.

Amesema wataendelea kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi,abiria na jamii kwa ujumla ili kujenga uelewa wa pamoja katika kuondokana na ajali ambazo zinaweza kuepukika.

Ameongeza pia wameweza kidhibiti ajali kwa kutumia mifumo ya ufuatiliaji wa mwendo kasi wa magari, VTS, na spidi Lada.