Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 09Article 541795

Habari Kuu ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Ajira walimu 6,900 ‘zaiva’

Ajira walimu 6,900 ‘zaiva’ Ajira walimu 6,900 ‘zaiva’

SERIKALI iko katika hatua za mwisho za kuajiri walimu 6,949 zilizotangazwa hivi karibuni; Amesema Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa9 TAMISEMI), Dk Festo Ndugange.

Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Mlalo, Abdallah Shangazi (CCM), Naibu Waziri Ndugange alisema serikali inaendelea kuratibu ajira za walimu 6,949 kwa nafasi za ajira zilizotangazwa Mei 2021 watakaopangwa katika shule mbalimbali zikiwemo za Wilaya ya Lushoto.

Katika swali lake Shangazi alisema kwa mujibu wa Ikama, Halmasauri ya Wilaya ya Lushoto ina upungufu wa walimu wa shule za msingi takribani 1,270.

Hivyo, Shangazi alitaka kujua mpango wa serikali wa kupeleka walimu katika halmashauri hiyo.

Akijibu swali hilo, Ndugange alisema katika kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2016/17 hadi 2019/20 serikali imeajiri na kuwapanga walimu 148 wa shule za msingi na walimu 118 wa shule za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto kati ya walimu 26,181 wa shule za msingi na sekondari walioajiriwa katika kipindi hicho.

Katika hatua nyingine, Dk Ndugange alisema azma ya serikali ni kujenga Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) katika kila wilaya.

Katika swali lake la msingi, Mbunge wa Liwale, Zuberi Kuchauka (CCM) alitaka kujua kama serikali iko tayari kuunga mkono juhudi za wananchi wa Kata ya Makata - Liwale ambao wameanzisha ujenzi wa chuo cha Veta na madarasa mawili yamekamilika.

Alisema serikali inatambua jitihada zinazofanywa na wananchi za kuona umuhimu wa kuwa na chuo cha ufundi stadi katika maeneo yao wakiwemo wananchi wa Kata ya Makata - Liwale.

"Azma ya serikali ni kujenga chuo cha ufundi Stadi katika kila wilaya nchini. Katika kutimiza azma hiyo, serikali inaendelea na ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi katika wilaya 29 nchini na kwa kuwa serikali inatekeleza mpango huu kwa awamu, nashauri wananchi wa Kata ya Makata waendelee na juhudi hizo wakati serikali inaendelea kutafuta fedha,” alisema.

Akaongeza: "Aidha, niombe uongozi wa wilaya uwasiliane na uongozi wa Veta kuona namna ya kupata msaada wa kitaalamu kuhusu ujenzi wa majengo ya vyuo vya ufundi stadi.”

Join our Newsletter