Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 22Article 573502

Uhalifu & Adhabu of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Akamatwa kwa tuhuma za mauaji, mwingine asakwa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Urlich Matei Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Urlich Matei

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Mbagala Wilaya ya Mbeya, Shizya Juma (32) maarufu Rais kwa tuhuma za mauaji ya Clement Salimo (40).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Urlich Matei amesema tukio hilo la mauaji limetokea Novemba 21 mwaka huu na kwamba mtuhumiwa baada ya kufanya tukio hilo alitoweka.

Matei amesema kuwa mtuhumiwa baada ya kukimbia Jeshi la Polisi liliendelea na msako na kufanikiwa kumkamata katika kijiji cha Ilomba Wilaya ya Mbozi mkoa wa Songwe baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema na kwamba alipohojiwa alikiri kuhusiana na tukio hilo pasipo kueleza sababu.

''Mtuhumiwa alikimbilia kujificha na kwa sasa Polisi wanaendelea na mahojiano ili waweze kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili''amesema

Katika hatua nyingine Kamanda Matei mesema kuwa Mkazi wa Kitongoji cha Kasakalawe Wilayani Chunya, Scacha anatafutwa na polisi kwa tuhuma za mauaji ya mchumbaji wa madini, Adam Jacob (31).

Matei amesema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni kumtuhumu marehemu kuhusika kimapenzi na mpenzi wake na kupelekea kuibuka kwa ugomvi uliopelekea mtuhumiwa kumchoka na kitu chenye ncha kali marehemu.

''Mtuhumiwa baada ya kuibuka kwa ugomvi alimchoma marehemu na kichu chenye ncha kali na kumsababishia jeraha lililopelekea kumwagika damu nyingi na hatimaye kupoteza maisha akiwa anapatiwa matibabu'''amesema.