Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 24Article 553432

Siasa of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Alichoandika Slaa muda mchache kabla ya kuhojiwa

Jerry Slaa, Mbunge wa Ukonga Jerry Slaa, Mbunge wa Ukonga

Mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe mfupi wa maneno unaosema ‘Hoja haizimwi kwa nyundo’.

Ameandika hayo leo Jumanne Agosti 24, 2021 muda mfupi kabla ya kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge huku akiambatanisha picha ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiashiria kuwa ndiye aliyeyasema maneno hayo.

“Hoja haizimwi kwa nyundo-Dr. Jakaya M Kikwete”

Slaa amewasili bungeni baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kuamuru yeye na Mbunge wa Kawe, Askofu Gwajima kuhojiwa na kamati hiyo kwa tuhuma za kusema uongo na kushusha hadhi ya Bunge.

Slaa amewasili bungeni saa 6:49 mchana akiwa kwenye gari jeusi huku mkononi akiwa na vitabu pamoja na sanduku jeusi.