Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 02Article 567472

Habari Kuu of Tuesday, 2 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Alichosema Rais Samia Glasgow leo

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia amesema Mabadiliko ya Tabianchi ni suala la Dunia nzima, hivyo suluhisho lake linapaswa kuwa la Ulimwengu wote.

Amesema ili kupambana na janga hilo la kidunia ni muhimu kwa mataifa yaliyoendelea kusaidia nchi maskini kifedha ili kuunganisha nguvu ya pamoja katika kudhibiti changamoto hiyo.

"Wote tunatambua nini kinahitajika, na nini kifanyike ili kuweza kukabiliana na janga hili la kidunia, ningependa kuziomba nchi zilizoendelea kuweza kusaidia mataifa yetu yanayoendelea kama nchi yangu Tanzania kupambana na janga hili, ni kweli hatuwezi kupambana na hili pasipo msaada wa kifedha kutoka kwa mataifa yaliyoendelea" Rais Samia.
Ameeleza kuwa hatua za pamoja zikichukuliwa na Mataifa, inawezekana kuokoa Ulimwengu