Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 26Article 544312

Diasporian News of Saturday, 26 June 2021

Chanzo: millardayo.com

Alichozungumza Rais Mwinyi juu ya Marathon ZNZ na Covid (+picha)

Alichozungumza Rais Mwinyi juu ya Marathon ZNZ na Covid (+picha) Alichozungumza Rais Mwinyi juu ya Marathon ZNZ na Covid (+picha)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kufanyika kwa Tamasha la Mashindano ya Kimataifa ya Marathon (Zanzibar International Marathon – ZIM ) hapa nchini, kutaonyesha utayari wa Serikali katika kuvutia Wawekezaji, hususan kupitia sekta ya Utalii.

Dk. Mwinyi amesema hyo Ikulu Jijini Zanzibar, alipozungumza na Viongozi, Wadhamini, Mabalozi na Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Mashindano ya Kimataifa ya Marathon (ZIM) yalio chini ya Uratibu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.

Amesema pamoja na tamasha hilo kuitangaza Zanzibar pia litaleta sura ya kuwahamasisha watu mbali mbali kuja kuona vivutio vya Utalii vilivyopo nchini na kuwekeza katika shughuli mbali mbali za kibiashara.

Alisema mchezo wa Marathon ni miongoni mwa mambo yenye kusisimua Utalii, hivyo akaahidi Serikali kuunga mkono hatua zote za maandalizi ya mashindnao hayo hadi kukamilika kwake.

Aliwashukuru waandaaji wa mashindano hayo na kubainisha furaha aliyonayo kutokana na wazo linalolenga kuutangaza Utalii wa Zanzibar, wakati huu Dunia ikikabiliwa na janga na maradhi ya Covid 19.