Uko hapa: NyumbaniHabari2021 12 15Article 578626

Habari Kuu of Wednesday, 15 December 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Alichozungumza Samia kuhusu kesi ya Mbowe

Freeman Aikael Mbowe, Mwenyeketi wa CHADEMA Freeman Aikael Mbowe, Mwenyeketi wa CHADEMA

Wakati Kesi ya Uhujumu Uchumi na Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe ikiendelea katika Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi, Rais Samia ameibuka na kusafisha njia kufuatia yale yanayoendelea juu ya msingi wa mashitaka hayo

Akishiriki Mkutano wa wadau wa kujadili hali ya demokrasia ya vyama vya siasa nchini amesema kuwa msingi wa kesi hiyo ni uvunjwaji wa sheria.

Samia amesema kuwa amekuwa akipokea maombi mengi kutoka kwa viongozi wengi wa vyama vya siasa wakimtaka amsamehe kiongozi huyo hivyo ameona azungumzie kuhusu suala hilo kwa undani.

"Yule mwenzetu ameshindwa kuheshimu demokrasia, kuheshimu demokrasia ni pamoja na kuheshimu sheria, unapovunja sheria za nchi hutaheshimiwa, mwisho wa uhuru wako ndio mwanzo wa heshima ya mwingine"

Akifafanua jambo hilo, Rais samia amesema kuwa Serikali haitaweza kuheshimu mtu anayevunja sheria kwa maslahi yake binafsi hivyo lazima sheria ifuate mkondo wake.

"Unapojiheshimu Serikali nayo itakuheshimu, na muelewe kuwa mtaka nyingi na saba hupata mwingi misiba, ingawa kusameheana kupo"

Amesisitiza na kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kusameheana na kufungua kurasa mpya ikiwa ni pamoja na kuzizika tofauti zote na kuanza upya ili kujenga Tanzania imara.