Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 29Article 540469

Uhalifu & Adhabu of Saturday, 29 May 2021

Chanzo: millardayo.com

Aliedaiwa kuwa ni jambazi auawa DSM (+video)

Aliedaiwa kuwa ni jambazi auawa DSM (+video) play videoAliedaiwa kuwa ni jambazi auawa DSM (+video)

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemuua Kilambo Nyasairo (44) mkazi wa Chanika mkoani Dar es Salaam kwa tuhuma za ujambazi.

 Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum DSM, Camillius Wambura amesema jana saa tano usiku mtuhumiwa huyo alikamatwa na baada ya kuhojiwa alikiri kujihusika na ujambazi na anamiliki silaha.

Amebainisha kuwa baada ya kupekuliwa aliwapeleka Polisi kuwaonyesha alipoifukia silaha lakini  wakati Askari wanachimba kuitoa, mtuhumiwa alianza kukimbia kuelekea kwenye maporomoko ya kingo za Bahari ya Hindi.

“Askari walipiga risasi hewani ili kumuonya  asimame lakini hakutii  aliendelea kukimbia na kusababisha askari kumpiga risasi mguu wa kulia akaanguka chini.” Wambura

“Askari waliendelea kuchimba eneo aliloonyesha na kufanikiwa kuipata bunduki aina ya S/GUN yenye namba S/NO.006074010/CAR 0009,”  Wambura

Join our Newsletter