Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 22Article 573400

Habari za Mikoani of Monday, 22 November 2021

Chanzo: mwananchidigital

Aliyejikata uume afariki

Aliyejikata uume afariki Aliyejikata uume afariki

Mkazi wa Kijiji cha Itolwa wilayani Chemba mkoani Dodoma, Juma Juma (34) amefariki dunia baada ya kuukata uume wake.

Inadaiwa kuwa Juma amefikia uamuzi huo wa kuukata uume wake baada ya kupata ajali na kuteguka kiuno na kusababisha asiwe rijali.

Akizungumzia juu ya tukio hilo Mwenyekiti wa kijiji hicho, Daudi Ally amesema leo Jumatatu Novemba 22, 2021 Juma amefariki baada ya kupungukiwa maji pamoja na damu.

Marehemu ameacha mjane mmoja na watoto watatu.