Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 18Article 552256

Uhalifu & Adhabu of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: MWANANCHI

Aliyemuua mkewe kwa kunyimwa unyumba akamatwa

Mtuhumiwa Kennedy Malekea akamatwa Mtuhumiwa Kennedy Malekea akamatwa

Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Kennedy Malekea (21), mkazi wa kijiji cha Msinga wilayani Rombo kwatuhuma za kumuua mkewe Fausta Silayo (22) kwa kumchoma visu vya tumboni na mgongoni kwa madai ya kunyimwa unyumba.

Marehemu Fausta alikuwa na mtoto mchanga wa mwezi mmoja alichomwa visu hivyo Julai 23 na kusababisha kifo chake Julai 24 alipokuwa akipelekwa hospitali ya Huruma kwa ajili ya matibabu.

Kamanda wa polisi Mkoa wa kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kukamatwa kwa Kennedy huyo baada ya kutoweka kwa siku 25 na kukimbilia nchi jirani ya Kenya baada ya kutenda tukio hilo.

"Ni kweli amekamatwa na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea," amesema Kamanda Maigwa.

Marehemu Fausta alizikwa katika kijiji cha Msinga wilayani Rombo kwa wazazi wake, Julai 31 mwaka huu ambapo ameacha watoto wawili mmoja ana umri wa mwezi mmoja na mwingine wa mwaka mmoja