Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 08Article 541582

xxxxxxxxxxx of Tuesday, 8 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Aliyeuawa na vijana wa JKT azikwa

Akizungumza kwenye shughuli hiyo, Dk Naano amesema sheria itachukua mkondo wake kwa kila mtu aliyehusika na mauaji hayo ya kulipiza kisasi kwa kuwa Serikali inathamini maisha ya kila Mtanzania.

"Hili tukio lisihusishwe na Serikali, hawa walioshiriki wamelifanya wao kwa matakwa yao, wala hakuna mtu aliyewatuma na ndio maana tayari tunawashikilia vijana watano na niwahakikishie tu kwamba haki lazima itatendeka, ingawa kijana wetu amefariki na hatuwezi kumrudisha," amesema Naano.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibishubwamu, amethibitisha kushikiliwa kwa vijana watano wa JKT kwa uchunguzi zaidi huku wakidaiwa pia kuwajeruhi watu wengine wawili kwa kipigo.

Join our Newsletter