Uko hapa: NyumbaniHabari2021 10 12Article 562810

Habari Kuu of Tuesday, 12 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Amuua kwa panga Mkewe

Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera Awadhi Juma Haji Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera Awadhi Juma Haji

Emmanuel Mdende (51) mkazi wa kijiji cha Mugajwale tarafa ya Rubale katika halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata kwa panga Mke wake Odiria Lucas (47) baada ya kumtuhumu kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera Awadhi Juma Haji amesema kuwa mauaji hayo yalitokea Oktoba 11 mwaka huu saa 8:45 mchana katika kijiji hicho, baada ya mtuhumiwa kumvamia mke wake wakati akiendelea na shughuli zake nyumbani na kisha kuanza kumkata kwa panga sehemu za shingoni.

"Wakati mama huyo akiendelea na shughuli zake nyumbani, mtuhumiwa alichukua panga na kumkata mara nne shingoni sehemu ya nyuma na kusababisha kifo chake papo hapo, hali hii inathibitisha kuwa alikusudia kuua" amesema Kamanda Haji