Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 18Article 558232

Uhalifu & Adhabu of Saturday, 18 September 2021

Chanzo: Mwananchi

Amuua mke kisa wivu wa mapenzi

Amuua mke kisa wivu wa mapenzi Amuua mke kisa wivu wa mapenzi

Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Ngulu, wilayani Mwanga, Kilimanjaro, Mwanaidi Hamisi amefariki dunia akidaiwa kukatwakatwa na panga sehemu mbalimbali za mwili wake kutokana na wivu wa mapenzi.

Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Abdallah Mwaipaya amesema tukio hilo limetokea Septemba 17, 2021 Kata ya Kwakoa.

Amesema wanandoa hao walikuwa wametengana kwa muda na Septemba 16 mwanaume huyo alimuomba mkewe watoke pamoja kujivinjari.

"Hawa wanandoa walikuwa wametengana kwa muda, juzi mwanaume akamwomba mkewe watoke ambapo alikubali ilipofika jioni mwanaume akamwomba arudi naye nyumbani kwake mwanamke akaridhia," amesema.

"Kumbe mwanaume alikuwa na nia ovu alipofika nyumbani akaanza kumkatakata kwa kutumia panga sehemu mbalimbali za mwili wake na baada ya kutenda tukio hilo alitoweka,"amesema Mwaipaya.

Mwaipaya amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini chanzo cha mauaji hayo.

Mwili wa mwanamke huyo umehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Same kwa taratibu za mazishi.