Uko hapa: NyumbaniHabari2021 07 13Article 546850

Habari za Mikoani of Tuesday, 13 July 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Amwagiwa Tindikali na Mwanaume Aliyemkataa

Amwagiwa Tindikali na Mwanaume Aliyemkataa Amwagiwa Tindikali na Mwanaume Aliyemkataa

Amwagiwa Tindikali na Mwanaume Aliyemkataa July 12, 2021 by cshechamboKABLA ya mkasa huu mzito, mwanadada Pramodini Roul ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 28, alikuwa mmoja wa mabinti warembo mno, lakini kilichompata ndipo ule usemi usemao duniani si mahali salama tena unapofanya kazi.

Pramodini, mkazi wa Jagatsinhpur, Odisha nchini India ameibuka na kusimulia mkasa wa kutisha wa kumwagiwa tindikali na mwanaume aliyekataa kuolewa naye.

Mwanadada huyo anasema kuwa, tindikali hiyo ilimharibu vibaya mno usoni na kichwani, lakini kama vile muujiza, ameolewa na mwanaume mwingine kwa jina la Saroj Sahoo mwenye umri wa miaka 29.

Kwa upande wake Saroj anasema kuwa, aliguswa mno na unyama aliofanyiwa mwanadada huyo kisha akawa anakwenda hospitalini mara kwa mara kumtembelea wakati huo akiuguza majeraha na kufanyiwa upasuaji wa aina mbalimbali kurekebishwa sura yake.

Anasema kuwa, tindikali aliyomwagiwa imemfanya mwanadada huyo awe na upara ambapo nywele haziwezi kuota tena.

Mwanaume aliyemuoa anasema kuwa, hana shida na kumuona sura yake ikiwa mbaya baada ya kufanyiwa upasuaji wa jicho la kushoto ambalo linaona kwa asilimia 20, lakini kabla ya hapo alikuwa haoni kabisa baada ya tindikali aliyomwagiwa na mwanaume aliyemkataa kumuoa.

Mwanadada huyo anasema kuwa, haamini kama bado duniani kuna watu wema kama mwanaume aliyemuoa kwani mwanaume huyo si tu kuwa amempenda alivyo na kilema alichosababishiwa, lakini pia mwanaume huyo aliacha kazi yake ya awali aliyokuwa akifanya ili wawe karibu zaidi.

Kwa sasa wote wameamua kufanya kazi katika shirika binafsi inayohusika kusaidia waathirika wa tindikali, “Nahisi kubarikiwa kuolewa na Saroj,” anasema mwanadada huyo wakati jamaa aliyemfanyia unyama huyo akisota gerezani.

Share this:TweetWhatsApp Related