Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 30Article 560524

Habari Kuu of Thursday, 30 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Anuani za makazi kuwekwa nchi nzima

Anuani za makazi kuwekwa nchi nzima Anuani za makazi kuwekwa nchi nzima

Serikali imewahimiza viongozi na watendaji wa serikali za mitaa, kwenda pamoja na juhudi zinazofanywa na serikali, kuweka mfumo wa anuani za makazi nchini kote.

Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji, wakati alipofungua semina ya kujenga uelewa na kuhamasisha utekelezaji wa mfumo wa Anuani za Makazi kwa Jumuiya ya Serikali za Mitaa.

"Hadi huu mwezi wa tisa mwaka 2021 ni asilimia tatu tu ya kata zote ndani ya taifa letu zilizofikiwa na huduma hii, kwa hiyo tukiangalia asilimia tatu ndani ya halmashauri 184 bado tupo nyuma, ndio maana tunataka tufanye zoezi hili kwa pamoja" Waziri Kijaji.

Amesisitiza juu ya mfumo huu, kuwa utarahisisha shughuli za kijami hasa kwa kwa kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja ikiwa ni pamoja na kurahisha upokeaji wa bidhaa.