Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 29Article 540580

Habari za Mikoani of Saturday, 29 May 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Askari Afa Maji Akimkimbiza Mtuhumiwa

Askari Afa Maji Akimkimbiza Mtuhumiwa Askari Afa Maji Akimkimbiza Mtuhumiwa

Askari Polisi, Isaya Kawogo amefariki dunia baada ya kuzama katika Ziwa Victoria wakati akimkimbiza mtuhumiwa wa ujambazi.

Hayo yameelezwa jana Ijumaa Mei 28, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibishubwamu akibainisha kuwa tukio hilo limetokea eneo la Mwisenge Manispaa ya Musoma.

Amesema askari huyo pamoja na wenzake wakiwa doria walikutana na mtuhumiwa huyo na kuanza kumkimbiza.

“Yule mtuhumiwa alijitosa ziwani na askari aliamua kumfuata huko huko ziwani lakini akiwa katika harakati za kumkamata alinasa kwenye nyavu na kuzama. Mtuhumiwa alifanikiwa kuimbia,” amesema Kamanda Tibishubwamu.

Join our Newsletter