Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 07Article 541507

Habari Kuu ya

Chanzo: millardayo.com

Askari JKT wakamatwa kwa tuhuma za mauaji

Askari JKT wakamatwa kwa tuhuma za mauaji Askari JKT wakamatwa kwa tuhuma za mauaji

Jeshi la Polisi Mkoani Mara linawashikilia Askari watano wa JKT kwa tuhuma za kumpiga hadi kumsababishia kifo Paulo Joseph(35).

Askari hao ambao walikuwa wakisubiri ajira baada ya kumaliza kipindi cha kujitolea walimtuhumu Paulo kumpiga Askari mwenzao.

Watu wengine watano walipigwa na Askari hao akiwemo Michael Mrema, Dereva wa gari la abiria inayofanya safari zake kati ya Bweri na Mjini kati.

Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Wananchi 27 KJ MAKOKO, Kanali Mushashi, ameahidi kushirikiana na wafiwa katika shughuli zote za msiba kwani waliohusika na mauaji wapo chini yake.

WOSIA WA TB JOSHUA KUELEKEA BIRTHDAY YAKE “HAITAKUWA RAHISI, SITOWEZA KUSHEREHEKEA”

Join our Newsletter