Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 09Article 541738

Habari Kuu of Wednesday, 9 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Askari Polisi wasiopewa kipaumbele kuneemeka 

Askari Polisi wasiopewa kipaumbele kuneemeka  Askari Polisi wasiopewa kipaumbele kuneemeka 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema wizara yake itakutana na wizara ya ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kuangalia uwezekano kuwapa Viwanja hususani kwa askari wa vyeo vidogo.

Simbachawene aliyasema hayo wakati kutoa maelezo ya ziada wakati wa maaswali na majibu.

Amesema, “Ni kweli askari ya Jeshi la Polisi wanafanya kazi nzuri kwa nchi yao, lakini kulingana na vyeo vyao ni ngumu kwa askari wa vyeo vya chini kujikomboa na kuwa na maisha mazuri baada ya kumaliza utumishi wao."

"Sisi kama wizara tunalichukua hili tujadiliane na wenzetu wa wizara ya ardhi kwani jambo hili ni jema na ni kweli wengine wanastaafu hawana hata nyumba wala kiwanja, tunalifanyia kazi tuone jinsi ya kuwapa viwanja hususani kwa askari under prevelage ( wasiopewa kipaumbele).

Katika swali lake la msingi, Mbunge Kaiza alitaka kujua ni kwanini Askari Polisi wasiwekewe utaratibu wa kusamehewa kodi katika vifaa vya ujenzi na kupewa viwanja kwa bei elekezi, ili wawe na moyo wa kulitumikia Taifa bila kujiingiza katika njia za udanganyifu kwa lengo la kujiandaa na maisha baada ya kustaafu.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri, Khamis Hamza Chilo alisema utaratibu wa utoaji wa msamaha wa kodi kwa bidhaa mbalimbali vikiwemo vifaa vya ujenzi kwa Askari wa Jeshi la Polisi ulikuwa unatekelezwa kupitia Sheria ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

Join our Newsletter