Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 20Article 558547

Uhalifu & Adhabu of Monday, 20 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Askari waliopambana na "Gaidi Hamza" watunukiwa fedha na vyeti

Kamanda Muliro awapa vyeti na Fedha askari walipambana tukio la Hamza Kamanda Muliro awapa vyeti na Fedha askari walipambana tukio la Hamza

Kamanda wa Polisi kanda ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema kuwa askari 11 waliopambana katika tukio la uhalifu uliofanywa na Hamza Mohamed amewapatia vyeti vya ujasiri pamoja na zawadi ya pesa kwa kadri alivyo ona inafaa.

Ametoa taarifa hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini humo na kusema kuwa askari hao walipambana kuhakikisha kwamba hakuna madhara makubwa yanajitokeza zaidi ya yaliyokuwa yamesha tokea katika tukio hilo.

"Askari Polisi walipambana kuhakikisha kwamba madhara makubwa zaidi ya yale yaliyotokea hayatokei, nani ambaye hafahamu kama yule mhalifu angeondoka na zile silaha zilizokuwa na magazine 2 na risasi 60 na zingine alizokuwa nazo nini kingefanyika"

"Askari hawa (Waliopambana na Hamza) miongoni mwao walikuwa ni Askari 11, ambao kwa mamlaka za kisheria za uendeshaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP amewapa zawadi ya vyeti vya ujasiri na zawadi ya pesa kwa kadri alivyoona inafaa"- Jumanne Muliro