Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 21Article 558838

Uhalifu & Adhabu of Tuesday, 21 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Askari waliovuka mipaka ya nchi wafukuzwa kazi Songwe

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Janeth Magomi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Janeth Magomi

JESHI la Polisi Mkoa wa Songwe limewafukuza kazi askari wake saba wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ileje mkoani humo kwa kosa la kuvuka mpaka na kuingia nchi jirani ya Malawi wakiwa na sare za Polsi na silaha za moto kinyume cha taratibu za kijeshi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Janeth Magomi amethibitisha kuwafuta kazi askari hao waliokuwa wakishikiliwa Malawi na baadaye kurejeshwa Tanzania.

Hivi karibuni askari hao waliripotiwa kutembezewa kipigo kutoka kwa raia wa Malawi, baada ya kuingia nchini humo wakidai kufanya operation ya kufuatilia pikipiki iliyodaiwa kubeba bidhaa za zilizodaiwa kuwa ni za magendo zilizoibiwa Tanzania.

Raia hao wa Malawi walikataa kutambua operation hiyo na kuwazingira kisha kuwashushia kipigo askari wakiwazania kuwa ni wahalifu huku gari lao likipigwa mawe na kuharibiwa vibaya.