Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 30Article 540637

Habari Kuu of Sunday, 30 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Askari wanyamapori wafundwa mahusiano binadamu na tembo

Askari wanyamapori wafundwa mahusiano binadamu na tembo Askari wanyamapori wafundwa mahusiano binadamu na tembo

JUMLA ya askari wanyamapori 20 kutoka wilaya ya Tunduru na Namtumbo mkoani Ruvuma wamepata mafunzo ya kujenga mahusiano kati ya binadamu na tembo.

Mafunzo hayo yalitolewa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyama pori Tanzania (TAWIRI) yakilenga kusaidia kuwajengea uwezo namna ya kutatua wa migogoro kati ya binadamu na wanyamapori.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dk Emmanul Masenga alitoa taarifa hiyo juzi kwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro.

Alisema licha ya kuwajenga uwezo, askari hao watatumika kufutiliaji,kufundisha wengine enye vijiji kulinda na kukabilina na matukio mbalimbali kwenye hifadhi na kutoa elimu kwa wananchi.

Dk Masenga alisema, mfumo huo unamtaka kila mshiriki wa mafunzo hayo walau kutoa elimu hiyo kwa wananchi mmoja kila mwezi.

Alisema,elimu hiyo itasaidia kupunguza mgongana na migogoro kati ya wanyamapori na binadamu na jamii kuacha kutumia mbinu za kizamani kama kupiga mayowe,kupiga madebe ambayo wakati mwingine imekuwa chanzo cha wanyamapori hususani tembo kujeruhi watu.

Ofisa Wanyamapori Mkuu kutoka Idara ya Wanyamapori Tanzania (TAWA), Dk Silvanus Okudo alisema, kwa kuwa wafugaji wanatumia nguvu ya fedha kuingia na kufanya shughuli zao kwenye hifadhi wamesababisha wanyamapori kwenda kwenye makazi ya wananchi na kufanya uharibifu .

Okudo aliomba serikali kuwa makini na kulipa uzito jambo hilo. Aliwataka askari hao kutumia elimu waliyopewa wakati wa kukabiliana na migogoro na changamoto nyingine watakazokutana nazo.

Mkufunzi wa mafunzo hayo , Dk Janemary Ntatwila alisema askari hao wamejengewa uwezo na mbinu za ulinzi wa mazao kwa kutumia uzio wa vitambaa na mafuta machafu, uzio wa pilipili na mizinga ya nyuki, tochi zenye mwanga mkali, honi , mabomu ya pilipili na matumizi ya fataki.

Akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mtatiro, alimewataka askari hao kutotumia mamlaka yao vibaya badala yake wamalize migogoro na muingiliano kati ya wanyamapori na jamii ili kumaliza changamoto iliyopo.

Aliomba wizara kuangalia upya sheria zake na kuangalia uwezekano wa kutumia bajeti zinazo tengwa na serikali kuchimba mabwawa kwenye maeneo ya hifadhi ili wanyama waweze kupata huduma hiyo badala ya kwenda kwenye maeneo yanayotumiwa na binadamu.