Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 25Article 553705

Uhalifu & Adhabu of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Askari watatu, mlinzi wa SGA wamepoteza maisha kwenye majibizano ya risasi DSM

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,  IGP Simon Sirro Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro

Jeshi la Polisi limesema idadi ya Watu waliouwawa na Mtu mwenye Bunduki aliekua akifyetua risasi ovyo karibu na Ubalozi wa Ufaransa Dar es salaam ni Watu wanne huku kati yao Watatu wakiwa ni Polisi na mmoja ni Mlinzi wa Kampuni binafsi ya ulinzi.

Haya yamethibittishwa na Kamanda Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simoin Sirro, mara baada ya tukio hilo kutokea liloacha athari kubwa kwa wanachi na wakazi ya maeneo hayo ya karibu.

"Leo August 25 2021 tumekutwa na tukio baya kabisa, tukio la kihalifu ambalo limepoteza maisha ya Watu wanne na watatu kati yao ni Askari Polisi, limetokea katika makutano ya barabara ya Kenyatta na Kinondoni Askari wetu walikua kazini akatokea Mtu akawashambulia kwa Bastola na alipowashambulia na kuanguka alichukua Bunduki za Askari hao na kuanza kurusha risasi ovyo kuelekea Ubalozi wa Ufaransa"-IGP,Sirro