Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 25Article 553645

Habari Kuu of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Askari wawili wameuawa kwenye majibizano ya risasi na jambazi DSM leo

Jeshi la Polisi limefanikiwa kumuua mtu aliyedhaniwa kuwa jambazi Jeshi la Polisi limefanikiwa kumuua mtu aliyedhaniwa kuwa jambazi

HALI ya taharuki imezuka katika eneo la Barabara ya Ali Hassan Mwinyi (karibu na Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa), zilizopo Kinondoni Jijini Dar es Salaam, baada ya watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kutaka kufanya uhalifu katika eneo hilo hii leo Agosti 25, 2021.

Tukio hilo lililodumu kwa zaidi ya saa moja, limepelekea kufungwa kwa barabara kuu ya Bagamoyo inayoingia na kutoka mjini huku baadhi ya magari yakiwa yameathiriwa kwa kupigwa risasi na mtu huyo.

Majambazi hao wamewaua Askari Polisi wawili na kuchukua bunduki mbili huku naye jambazi mmoja akiuawa katika majibizano ya risasi. IGP Simon Sirro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Inaelezwa kuwa jambazi huyo aliwashambulia na kuwadhuru polisi waliokuwa kwenye makutano ya barabara karibu na lilipo daraja la Selander pamoja na askari waliokuwa wakilinda ubalozini hapo.

Zikiwa ni saa chache tu zimepita tangu Rais Samia atoe kauli kuhusu watu waliokuwa wakiijaribu serikali ya awamu ya sita kwa matukio ya ujambazi kudhibitiwa huku kamanda mkuu wa Jeshi la Polis, Simon Sirro akitoa takwimu juu ya kupungua kwa matukio ya uhalifu, tukio hili linathibitisha utdhibiti wa jeshi la polisi katika kupambana na matukio ya ujambazi.