Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 22Article 552982

Siasa of Sunday, 22 August 2021

Chanzo: MWANANCHI

Askofu Gwajima: Nitakwenda kamati ya Bunge kusema ukweli

Mbunge wa kawe na Askofu  wa kanisa Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima Mbunge wa kawe na Askofu wa kanisa Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima

Mbunge wa Kawe na Askofu wa Kanisa Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amekiri kupokea barua ya wito wa kuitwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Jana, ilisambaa mitandaoni barua ya ofisi ya Bunge ikionyesha Gwajima na mbunge wa Ukonga, Jerry Slaa wanatakiwa kwenda mbele ya kamati hiyo Agosti 23 na 24.

“Nimepokea barua ya Spika kwenda kwenye kamati, nitakwenda. Nimesema hapa kwa kuwa aliyenitumia barua ameweka mitandaoni akisema kwanini nimesema hapa na yeye aniambie kwa nini aliweka mitandaoni,” amesema Gwajima , Agosti 22, 2021 alipokuwa akizungumza na waumini wake katika kanisa hilo, Dare es Salaam.

Askofu Gwajima amesema atakwenda kwenye kamati hiyo na atasimamia ukweli kama ambavyo imani yake inamtuma.

“Nitakwenda kwenye kamati wategemee ukweli nitasema ukweli kwa kuwa imani ya CCM ni ukweli na nitaongeza mengine ambayo sijawahi kusema. Lazima tusimamie nchi na watoto wa watoto wetu,” amesema askofu Gwajima.