Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 25Article 544189

Uhalifu & Adhabu of Friday, 25 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Aua mke na mtoto chanzo wivu wa mapenzi

Aua mke na mtoto chanzo wivu wa mapenzi Aua mke na mtoto chanzo wivu wa mapenzi

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga shoka kichwani na kumnyonga hadi kufa mtoto wao mwenye umri wa miaka miwili.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoani humo, Saphia Jongo, amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa baada ya kufanya mauaji hayo, mtuhumiwa aliwamwagia mafuta marehemu na kuwasha moto kwa lengo la kupoteza ushahidi.

Aidha, Kamanda Jongo amesema majirani waliojitokeza kutoa msaada baada ya kuona moto ndio waligundua mauaji hayo.

Diwani wa Ikomwa katika Manispaa ya Tabora, Salum Msamazi, amesema kuwa mwanamke huyo aliyeuawa alikuwa mjamzito.