Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 09Article 556498

Uhalifu & Adhabu of Thursday, 9 September 2021

Chanzo: ippmedia.com

Auawa kwa mapanga akizini na mke wa mtu kwenye zizi la ng'ombe

amanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi, Marrison Mwakyoma amanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi, Marrison Mwakyoma

MKAZI wa Kijiji cha Magara katika Wilaya ya Babati mkoani Manyara, Michael Jackson (25) amepoteza maisha, baada ya kuuawa kwa kucharangwa mapanga, alipokutwa akizini na mke wa mtu kwenye zizi la ng’ombe.

Mauaji hayo ya kulipiza kisasi yanadaiwa kutekelezwa na Samweli Alfred (48) ambaye ni mume wa ndoa wa Habiba Saidi (22).

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi, Marrison Mwakyoma, mauaji hayo yalifanyika jana kijijini hapo majira ya saa 10:00 alfajiri.

“Kutokana na tukio hilo, tunamshikilia mtuhumiwa wa maujai hayo aitwaye Samweli Alfred kwa ajili ya mahojiano zaidi.Kabla ya mauaji hayo zipo taarifa kwamba Alfred alimuaga mkewe (Habiba) akiwa kitandani amelala, akimweleza anakwenda kukata kuni.

“Lakini ghafla mkewe huyo naye, akatumia nafasi hiyo kumpigia simu na kumuita hawara yake marehemu Michael Jackson ili wafanye mapenzi.

Baada ya Michael kufika, walizunguka kwenye banda la ng’ombe na kutandika shuka la Kimasai maarufu kama mgorori chini na kuanza kufanya mapenzi ila ghafla mumewe (Alfed) alirejea na kuwafumania.”

Kamanda Mwakyoma, amesema Alfred kwa sababu alikuwa na panga alimkata sehemu mbalimbali za mwili mgoni wake Michael na kumsababishia kifo.

Baada ya kumcharanga kwa mapanga marehemu hadi kupoteza maisha, mtuhumiwa wa mauaji hayo alimgeukia mkewe (Habiba) aliyekuwa akimzuia asimuue hawara yake, naye alijeruhiwa vibaya kwa kukatwa mkono na kuudondosha chini.

“Tunaendelea na upelelezi na tunatarajia kumfikisha mahakamani wakati wowote Alfred, baada ya uchunguzi kukamilika,” amesema Mwakyoma

Aidha, Kamanda Mwakyoma ametoa wito kwa jamii ya eneo hilo kuwa waoga katika kutembea na wake za watu kwani wivu wa mapenzi ni matukio yanayojitokeza mara kwa mara.

“Aliyeuawa ana miaka 25 na mwanamke ana miaka 22 mume aliyefumania ana miaka 48. Wananchi wanatakiwa kuacha mapenzi yasiyo na tija kila mmoja achukue tahadhari,” amesema Mwakyoma

Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Magara, Ally Ramadhan, amesema Michael ambaye bado ni kijana, alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Habiba kwa muda mrefu na alionywa mara nyingi hakusikia.