Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 15Article 542722

Habari za Mikoani of Tuesday, 15 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Aweso amtengua Mkurugenzi Mtendaji wa maji Sengerema

Aweso amtengua Mkurugenzi Mtendaji wa maji Sengerema Aweso amtengua Mkurugenzi Mtendaji wa maji Sengerema

Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 14, 2021 na Wizara hiyo na imeeleza kuwa kabla ya uteuzi huo Sadala Hamis alikuwa ni mtumishi katika Wakala wa Maji na Usafi Mazingira Vijijini (Ruwasa).

"Waziri Aweso amefanya uteuzi huu kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa sheria ya huduma za maji na usafi wa mazingira, sheria namba 5 ya mwaka 2019. Lupoja atapangiwa majukumu mengine," imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa katika hatua nyingine, Aweso ameivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Sengerema huku taratibu nyingine zikiendelea kufanyiwa kazi.