Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 27Article 540058

xxxxxxxxxxx of Thursday, 27 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

BARA, ZANZIBAR KUGAWANA NAFASI ZA AJIRA

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa umelenga kuwawezesha wananchi kuishi kwa amani na utulivu kuharakisha kasi ya maendeleo.

Aidha, Dk Mwinyi alisema jana kuwa serikali imelipatia ufumbuzi suala la uwiano wa nafasi za ajira kati ya vijana wa Tanzania Bara na Zanzibar kupitia vikao vya kamati ya masuala la Muungano.

Taarifa ya Ikulu jana ilileza kuwa Zanzibar itapata wastani wa

asilimia 21 ya nafasi hizo zitakazotangazwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dk Mwinyi aliyasema hayo Ikulu mjini Unguja alipozungumza na uongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora uliokwenda ofisini kwake kumsalimu.

Alisema uundaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa umeleta ufumbuzi wa changamoto za kisiasa zilizokuwa zikiikabili Zanzibar.

Dk Mwinyi alisema serikali inakusudia kuweka nguvu zaidi katika kuyapatia ufumbuzi matatizo ya wananchi yanayowasilishwa kwake, kutekeleza ahadi alizozitoa

wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Alipongeza juhudi za tume hiyo kuweka mfumo mzuri wa mawasiliano ya kimtandao na kuwafikia wananchi wengi zaidi hasa kutokana na ukubwa wa nchi ya Tanzania.

Aliahidi kulipatia ufumbuzi tatizo la ofisi za tume hiyo Unguja na Pemba ili itekeleze majukumu yake kwa ufanisi.

Awali, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania, Jaji mstaafu Mathew Mwaimu alisema tangu Dk Mwinyi achaguliwe kuiongoza

Zanzibar, amethibitisha nia ya dhati ya kuwaunganisha Wazanzibari baada ya kushirikiana na Chama cha ACT Wazalendo na kuunda Serikali ya Umoja wa kitaifa.

Jaji Mwaimu alisema hatua hiyo imesaidia Zanzibar kuwa tulivu na wananchi bila kujali vyama vyao vya kisiasa wanashirikiana kuleta maendeleo na kuwezesha serikali kufikia uchumi wa bluu.

Alimpongeza Dk Mwinyi kwa juhudi za kupambana na vitendo vya rushwa, kusimamia matumizi ya mapato ya serikali na hatua za kuwawajibisha viongozi wasiozingatia utawala bora.

Join our Newsletter