Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 04Article 583186

Habari Kuu of Tuesday, 4 January 2022

Chanzo: www.mwananchi.co.tz

#BREAKING NEWS: Tisa wafa boti ikizama Pemba

Tisa wafa boti ikizama Pemba Tisa wafa boti ikizama Pemba

Watu tisa wamefariki dunia na wengine kadhaa kuokolewa baada ya boti waliokuwa wakisafiria kuzama Mkoa wa Kusini Pemba.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Matar Zahor Masoud amesema ajali hiyo imetokea leo Jumanne Janauri 4, 2022 jioni wakati watu hao wakitokea Chakechake kwenda Kisiwa Panza msibani, moja ya vyombo vilivyotumika kuwavusha kimepata hitilafu na kuzama.

"Mpaka sasa maiti tisa zimeopolewa zipo hospitali ya Mkoani kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kidaktari ili baadaye taratibu za kukabidhi familia zao sitaendelea," amesema

"Kwahiyo kwa wenzetu wa vyombo vya ukozi kwa maana ya KMKM (Kikosi Cha kuzuai Magendo) na wananchi walikuwa wakiendelea na zoezi hili lakini kutokana hali ya maji na kiza kazi hiyo tumeiahirisha tutaendelea nayo asubuhi mapema sana kuangalia kama kuna maiti nyingine au watu walionusurika tuweze kuwaokoa" amesema

Amewaomba wananchi kutoa ushirikiano na kuendelea kuwa na uvumilivu Serikali itatoa taarifa zaidi baadaye.

Amesema hawajapata taarifa za chanzo cha ajali lakini taarifa za awali zinadai huenda ikawa ni idadi kubwa ya watu waliokuwa ndani ya boti hiyo kwasababu hakuna uhakika walikuwa watu wangapi lakini ni kwamba walikuwa wanazidi watu 30.