Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 15Article 585928

Habari Kuu of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Baba Aliyechinjwa na Mwanaye Mwanajeshi Azikwa - Video

Baba Aliyechinjwa na Mwanaye Mwanajeshi Azikwa - Video play videoBaba Aliyechinjwa na Mwanaye Mwanajeshi Azikwa - Video

MWILI wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi Taifa (CCM), Edward Ndonde anayedaiwa kuuawa kikatili kwa kuchomwa visu na mtoto wake, Mussa ambaye ni mtumishi wa Ruvu JKT umezikwa jana nyumbani kwake Mbeya.

Simanzi, majonzi na vilio vimetawala miongoni mwa waombolezaji wakati wa maziko ya Mzee Ndonde jana Ijumaa, Januari 14, 2022 ambayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema mtuhumiwa ambaye ni mtumishi wa Ruvu JKT, alikamatwa baada ya kufanya mauaji hayo Jumatano Januari 12, 2022 na uchunguzi unaendelea ili hatua za kisheria ziweze kushika mkondo wake.