Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 27Article 540184

Habari Kuu of Thursday, 27 May 2021

Chanzo: ippmedia.com

Baba yangu ni mzima wa afya -Ridhiwani

Ridhiwani amekanusha taarifa hiyo leo Alhamis Mei 27, 2021 kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya kupokea simu na jumbe mbalimbali wakitaka uhakika wa taarifa hizo.

"Baada ya kupokea simu na jumbe mbalimbali nimeona nitumie nafasi hii kuweka kumbukizi sawa. Mzee wetu na Mzazi wetu Dk Kikwete yupo salama wa afya nyingi sana. Hana tatizo lolote kiafya na anaendelea na majukumu yake. Taarifa za aina yeyote ni za kipuuzi na za kupuuzwa.” ameandika Ridhiwani.