Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 07Article 541567

Habari Kuu of Monday, 7 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Balozi Mulamula afanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia

Balozi Mulamula afanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Balozi Mulamula afanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia

Mazungumzo hayo yamefanyika leo Juni 7, katika Ofisi ya Waziri Mulamula jijini Dodoma, ambapo Waziri huyo amesema mahusiano hayo yamelenga kunufaisha miradi ya maendeleo nchini.

Akiongelea uhusiano baina ya Tanzania na Benki ya Dunia Balozi Mulamula amesema Tanzania imejipanga kuhakikisha mahusiano kati ya Tanzania na Benki hiyo yanaimarika na kuendeleza uwezo wa Watanzania wanaosimamia miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Benki ya Dunia ikiwa ni pamoja na kuendeleza sekta binafsi na kuifanya kuwa imara.

“leo hapa tumejadiliana juu ya mahusiano yetu, kuangalia namna ya kuyaboresha ili kunufaika na miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Benki hiyo, kuwajengea uwezo watu wetu wanaosimamia utekelezaji wa miradi hiyo na uimarishaji wa Sekta binafsi ili kuwa imara na hivyo kufikia maendeleo ya kweli,” amesema Balozi Mulamula.

Akiongelea kuhusu mipango ya Serikali ya kuimarisha Sekta Binafsi Mhe Waziri Mulamula amemuhakikishia Dkt. Taufilo nia na mtizamo wa Serikali wa kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara na kuwekeza nchini ikiwa ni pamoja na kushirikiana na sekta binafsi hasa ikizingatiwa kuwa Benki ya Dunia inachukulia sekta binafsi kama chachu ya maendeleo na hivyo kuwa na miradi ya kusaidia ukuzaji wa Sekta binafsi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji huyowa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika kundi la kwanza Dkt. Taufila Nyamadzabo amesema miongoi mwa mambo waliyojadili leo ni pamoja na umuhimu wa kuhusisha sekta binafsi na kuiendeleza.

Join our Newsletter