Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 26Article 544255

Siasa of Saturday, 26 June 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Baraza la wazee Mkoa wa Dar Wambariki Katibu Wa CCM

Baraza la wazee Mkoa wa Dar Baraza la wazee Mkoa wa Dar

Mwenyekiti wa baraza hilo, Mohammed Mkali (kulia) akizungumza na waanahabari. Kushoto ni Mohammed Mtulia.

BARAZA la Wazee la Mkoa wa Dar es Salaam, limembariki Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa mkoa huo, Shaibu Akwilombe na kuahidi kumpa ushirikiano wa kutosha.Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa mkoa huo, Shaibu Akwilombe akizungumza.

Hayo yamesemwa wakati wa hafla ya Akwilombe kujitambulisha kwa wazee hao , jijini Dar es Salaam, ambapo baraza lilimhakikishia ushirikiano katika kukijenga chama.

Akizungumza kwa niaba ya wazee wa mkoa huo, Mwenyekiti wa baraza hilo, Mohammed Mkali, alisema hata kabla ya Akwilombe kujitambulisha, wazee mkoani humo wameridhishwa na kasi ya utendaji wake aliyoanza nayo.

“Tunaomba uendelee na kasi hiyo. Wazee tuko pamoja na wewe katika kutekeleza Ilani ya CCM na kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza Ilani hiyo,”alisema Mkali.

Kwa upande wake Akwilombe, aliahidi kushirikiana na wazee hao na kwamba Baraka zao zinamfanya kupata faraja ya kuendeleza mapambano katika kukipigania Chama.