Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 13Article 585406

Habari Kuu of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Bashungwa: Watumishi TAMISEMI hudumieni kwa wakati, ubora

Innocent Bashungwa, Waziri TAMISEMI Innocent Bashungwa, Waziri TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofi si ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa (pichani) amesema wizara hiyo si ngumu kama watumishi wote watashirikiana na kuwahudumia wananchi kwa wakati na ubora.

Alisema hayo wakati wa makabidhiano ya ofisi kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu katika jengo la Sokoine mjini hapa. “Tamisemi si ngumu kama watumishi wote watajenga mahusiano bora na kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa wakati na kutatua changamoto za wananchi kwa wakati na ubora,” alisema.

Bashungwa aliwataka watumishi wa Tamisemi kuendelea kushirikiana katika kufanyakazi na kuwa na mshikamano kwa kuwa lengo kuu ni kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia wananchi na taifa kwa ujumla. Kwa upande wake, Ummy aliishukuru Menejimenti na watumishi wa Tamisemi kwa ushirikiano walioonyesha kipindi alipokuwa akihudumu katika ofisi hiyo.

Alisema Tamisemi sio ngumu bali ni kubwa kutokana na kuwa na uwanja mpana wa kufanyia kazi. “Tamisemi ni kubwa kwa kuwa inakupa uwanja mpana wa kuchagua jinsi gani utakavyoweza kufanyakazi kwa kushirikiana na watendaji wengine ili kukamilisha malengo yaliyopangwa katika kutatua changamoto na kuboresha huduma katika jamii.”

Ummy aliwataka watumishi wa Tamisemi kutoa ushirikiano kwa Bashungwa ili aweze kutimiza majukumu yake kikamilifu. Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi anayeshughulikia elimu, David Silinde alimshukuru Ummy kwa kufanyakazi kwa muda wa miezi tisa katika wizara hiyo, lakini ameacha alama isiyofutika kwa jamii, ambayo ni ujenzi wa madarasa 15,000 ndani ya miezi miwili, kuongeza bajeti ya Tarura kutoka Sh bilioni 273.5 hadi Sh bilioni 966, ujenzi wa vituo vya afya na hospitali za halmashauri.

Naye Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – Tamisemi anayeshughulikia afya, Festo Dugange alimshukuru Ummy kwa kufanyakazi kwa ushirikiano na kuwa mmoja ya walioleta mabadiliko katika utendaji kazi wa Tamisemi ndani ya miezi tisa