Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 13Article 585463

Muziki of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Beka akerwa kufutiwa nyimbo Youtube

Beka akerwa kufutiwa nyimbo Youtube Beka akerwa kufutiwa nyimbo Youtube

Mkali wa muziki wa Bongo fl eva, Bakari Katuti ‘Beka Flavour’ amesema kitendo cha kufutwa nyimbo zake mbili za ‘Libebe’ na ‘Sikinai’ kwenye mtandao wa Youtube, kimemvunja moyo.

Beka Flavour ambaye aliwahi kutamba na kundi la Yamoto Band chini ya Said Fella, amesema kitendo hicho hakifurahishi na kinapaswa kukemewa na mamlaka.

Akizungumza na gazeti hili jana, Beka Flavour alisema kitendo hicho kimemsikitisha kwani hakina lengo zuri kwa muziki wake pamoja na Bongo fleva ambayo sasa imekuwa ikifanya vizuri duniani.

“Bado sijajua ni nani amefanya kitendo hiki na amefanya hivi akiwa na lengo gani, nashukuru mtandao wa Youtube wameniambia kuwa video zangu zimefutwa na mmoja wa watu ninaofanya nao kazi,” alisema Beka Flavour.

Alisema kamwe hataacha kufanya kazi ya muziki ambayo imemfanya ajulikane Afrika na duniani kwa ujumla na anawaomba mashabiki wake waendelee kumpa sapoti katika kazi zake ambazo anatarajia kuanza kuziachia mwaka huu.