Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 19Article 552499

Habari Kuu of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Benki ya Dunia kuipa Tanzania Bilioni 384.9, kubadili mifumo ya digitali

Mapinduzi ya kidigitali Mapinduzi ya kidigitali

Waziri wa Mawasiliano, Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Benki ya Dunia inatarajia kutoa dola za Marekani milioni 150 sawa na bilioni 384.9 za kitanzania, kwa ajili ya kuwezesha mabadiliko ya kidijitali nchini Tanzania.

Pamoja na mambo mengine, fedha hizo zitaboresha upatikanaji wa huduma za intaneti kwa ajili ya serikali, biashara na wananchi ili kukuza uwezo wa serikali kutoa huduma kwa njia za kidijitali.

Ameyabainisha haya wakati wa kikao cha mapitio ya maboresho ya kanuni za maudhui ya utangazaji na leseni, kilichofanyika mapema hii leo kikijumuisha Wizara hiyo pamoja na Wizara ya Habari.