Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 06Article 541303

Habari Kuu ya

Chanzo: millardayo.com

Benki ya Dunia yaidhinisha Trilioni 2 kwa Tanzania

Benki ya Dunia yaidhinisha Trilioni 2 kwa Tanzania Benki ya Dunia yaidhinisha Trilioni 2 kwa Tanzania

Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia (WB) imeidhinisha mikopo ya masharti nafuu yenye thamani ya Sh2.3391 trilioni kwa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa miradi minne ya maendeleo.

Hayo yamesemwa  Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba wakati akizungumza na waandishi wa habari siku moja kabla ya kuwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Dkt. Mwigulu amesema mradi iliyopitiwa fedha hizo ni ya uboreshaji wa barabara za vijijini na fursa za kijamii (RISE), mradi wa kuimarisha mazingira ya ufundishaji na mafunzo katika taasisi za elimu ya juu (Heet).

Miradi mingine ni wa kusaidia kuongeza upatikanaji wa huduma za mtandao (DTP) na mradi wa kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma bora na za uhakika za Umeme Zanzibar (Zesta).

UKWELI KIFO CHA TB. JOSHUA, AMEFARIKI PUNDE BAADA YA IBADA, ALIYOSEMA YALITABIRI KIFO CHAKE

Join our Newsletter