Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 25Article 559591

Habari Kuu of Saturday, 25 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Biashara ya Ukahaba Itakomaje Dar?

Makahaba baada ya kukurupushwa na polisi. Makahaba baada ya kukurupushwa na polisi.

MKUU wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Amos Makalla ameagiza biashara ya ukahaba ikome; Mkuu wa Mkoa anasema ni kuwakamata wote wanaojihusisha na biashara hiyo haramu huku walengwa wakuu wakiwa ni wanawake.

Hata hivyo; mjadala wa agizo la mkuu wa mkoa ulikuwa juu ya ushauri wake aliowataka polisi ikibidi waende kijasusi maeneo ya “soko la ukahaba” wakiwa wamevalia mavazi ya kiraia.

Lakini watu wanasema; askari hao wakifika huko wafanyaje kwa mfano ili wapate ushahidi wa tukio?

Maana kumkuta mtu kasimama kwenye kichaka haimaanishi ni kahaba, ni gumzo zito, lakini ukweli unabaki kuwa biashara ya ukahaba ni haramu kwenye nchi yetu.

Ingawa wengine wanauliza, Jinai isiyokuwa na sheria inawezaje kukomeshwa?

Maana mkanganyiko wa kisheria upo; kwamba mwanamke anapokamatwa usiku kwenye maeneo yanayoitwa ya kujiuza akifikishwa mahakamani anafunguliwa shtaka la uzembe na uzururaji kwa sababu sheria ya kumbana juu ya ukahaba imepindapinda.

Kusema kweli tatizo hili linafikirisha jinsi ya kulimaliza na wengine wamefika mbali kifikra kwamba pengine ukahaba ungehalalishwa tu na hao wanaofanya kazi hiyo waanze kulipa kodi kama ilivyo kwenye mataifa mengine,

Ukilifikiria hili nalo unaona lina ukakasi, hii sio sawa mila tamaduni na desturi haziruhusu hata vitabu vya dini lakini bado ukahaba ni biashara ambayo inawauzaji wa kutosha na wanunuaji wa kutosha.

Hebu tujadili; dawa ya ukahaba jijini Dar ni nini na biashara hii itakomaje?