Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 09Article 541903

xxxxxxxxxxx of Wednesday, 9 June 2021

Chanzo: millardayo.com

Big Joe Kusaga atoa mchongo wa Milioni 550

Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group Joseph Kusaga leo anasherehekea kufikisha umri wa miaka 55 na ameamua kutangaza mchongo mkubwa wa Taifa leo kwenye siku yake kubwa ambao unathamani ya milioni 550 Tsh.

Namshukuru sana Mungu kwa kunipa nafasi ya kuwaongoza CMG, katika kuangalia na kuona kuna biashara nyingi na Vijana wengi ambao wana biashara lakini bahati mbaya hakuna kitu chenye gharama kama kutangaza biashara”———CEO wa CMG Kusaga

“Katika kufikiri nikasema hii miaka yangu 55 kwanini nisichague tena Vijana 55 ambao watakuwa na matangazo yenye thamani ya Tsh. Milioni 10 kwa kila kijana yawe ya mwezi mzima na hayo matangazo yatakuwa na thamani ya Tsh. Milioni 550”———Kusaga

“Big Joe Incubator nia yangu ni kuhakikisha kwamba tunafanya kitu ambacho kitafungua milango kwa Watu wengi, itanyanyua middle class na hawa Vijana 150 watainua Watu wengine na tutawabeba kwa ukubwa”———-Kusaga

“Big Joe Incubator ni project nashirikiana na wadau wengi tofauti ambao wamekubali mawazo yangu ya mimi kufungua milango kwa zaidi ya Vijana 150, hasa wanaojihusisha na techonology lakini wanakosa support ya mafunzo na funds”———Kusaga

TUKIO LOTE LA RAIS MACRON KUZABWA KOFI MBELE YA WALINZI, “HAIKUPANGWA AWE PALE”

Join our Newsletter