Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 24Article 559504

Habari za Afya of Friday, 24 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Bila Chanjo ni marufuku kuingia Marekani kuanzia November

Bila Chanjo ni marufuku kuingia Marekani kuanzia Novemmber Bila Chanjo ni marufuku kuingia Marekani kuanzia Novemmber

Serikali ya Marekani imetangaza sharti jipya na gumu kwa watu wanaosafiri kuingia nchini humo kwa shughuli za kibiashara, matembezi au familia.

Taarifa ya Ubalozi wa Marekani nchini Kenya imesema kuwa kutakua na sheria kali kwenye suala la uingiaji nchini humo kuanzia mwenzi November 2021.

Kaimu Balozi wa Marekani nchini Kenya, amesema kuwa mtu yeyote anayetaka kuingia nchini Marekani kuanzia mwezi November mwaka huu ni lazima awe na cheti cha kupata chanjo ya COVID-19.

Watakaoruhusiwa kuingia bila sharti hilo ni raia wa Marekani na wale wenye kibali cha ukaazi (Green Card).

Akizungumza na kituo cha Radio cha Capital FM nchini Kenya Balozi Fertik amesema kuwa serikali ya Marekani inatarajia kupendekeza ni aina gani ya chanjo itakua na ruhusu kwa mtu kuingia Marekani.