Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 23Article 553099

Habari Kuu of Monday, 23 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Bila haki nchi itavurugika"- Mtendaji Mkuu Mahakama

Prof.Elisante Ole Gabriel Prof.Elisante Ole Gabriel

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof, Elisante Ole Gabriel, amewataka Watendaji wote wa mahakama kuzingatia maadili ya kazi zao ili kupunguza mlundikano wa kesi katika Mahakama.

Amewataka kufanya kazi kwa bidii ili kufkia malengo makuu ya Mahakama ikiwa nipamoja na kuwapa watu haki zao ndani ya muda sahihi.

"Mahakama ni Taasisi kubwa ya kutoa haki, hivyo tuna kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha tunawapa watu haki zao, bila haki nchi itavurugika"

Aidha amewasihi watumishi wote wa mahakama kujenga utamaduni wa kupenda wanachokifanya, kudumisha umoja na upendo kati yao,ili kufikia malengo makuu ya Mahakama.